SAYANSI MWAKA WA KWANZA (I)

WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
CHUO CHA UALIMU ILONGA
IDARA YA SAYANSI
MASWALI YA NYUMBANI MWAKA WA KWANZA NOV, 2023
 
Kazi ya kufanya likizo kwa mwaka wa pili.

Imetolewa tarehe 26/11/2023
Sir Godfrey Steven
 
1. (a) Eleza kwa kifupi maana ya kujifunza.
(b) Bainisha kazi 3 anazotakiwa kuzifanya mwalimu darasani ili kumsaidia
mwanafunzi aweze kujifunza.
 
2. Taja vitendo 5 vinavyoweza kufanywa na wanafunzi ili waweze kupimwa na
mwalimu wao.
 
3. (a) Ili msingi wa kufundishia somo la Sayansi wa “Kutenda vitendo katika
ufundishaji na ujifunzaji” ufanikiwe, ni mambo gani yanatakiwa
kuzingatiwa?.
(b) Nini maana ya kujifunza kwa “ujenzi wa maana”?
 
4. (a) Eleza maana ya kufundisha.
(b) Kwa kutumia mifano, bainisha mitazamo ya ujifunzaji. (Toa mfano mmoja
kwa kila mtazamo).
 
5. (a) Tofautisha uchunguzi wa kisayansi na jaribio la kisayansi.
(b) Andika ripoti ya jaribio la kisayansi lililofanywa la kuonesha mabadiliko
katika hali za maada kiumbo.
 
6. Eleza hatua kwa hatua namna ya kufundisha kwa njia ya jarbio ili wanafunzi
waweze kuelewa.
 
7. Kwa kutumia michoro onesha ni nini hutokea wakati
a) Mwanga unaposafiri kutoka media moja hadi nyingine zenye ujazonene
tofauti
b) Miale ya mwanga inapopita kwenye lensi mbinuko
 
8. Eleza kwa ufupi maana ya istilahi zifuatazo
a) Omnivora
b) Hebivora
c) Kanivora
d) Kinga ya mwili
 
9. Kuungua kwa karatasi ni badiliko la kemikali. Thibitisha kauli hiyo kwa
kutoa hoja nne.
 
10. Gurudumu na ekseli zenye ufanisi wa 95% ilitumika kuinua mzigo wenye
uzito wa 1200N. Ikiwa nusu kipenyo cha gurudumu ni sm 40 na cha ekseli
ni sm 5. Kokotoa
a) Uwiano wa mwendo dhahiri wa gurudumu na ekseli
b) Manufaaa ya kikenika
c) Jitihada iliyotumika kuinua mzigo
 
11. (a) Maabara ni nini?
b) Eleza sifa 5 za maabara bora
c) Taja alama tano za tahadhali za kemikali zinazotumika katika chupa za
kuhifadhia kemikali mbalimbali katika maabara
d) Eleza tahadhari 4 za kuchukua ili kujikinga wewe mwenyewe na ajali
katika maabara.
 
12. Kwa kutumia mifano, bainisha njia nne zinazoweza kueneza magonjwa ya
kuambukiza.

13. (a) Eleza maana ya ukinzani katika umeme
(b) Taja sababu tatu (03) zinazoathiri ukinzani katika umeme
{"name":"SAYANSI MWAKA WA KWANZA (I)", "url":"https://www.quiz-maker.com/QPREVIEW","txt":"WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIACHUO CHA UALIMU ILONGAIDARA YA SAYANSIMASWALI YA NYUMBANI MWAKA WA KWANZA NOV, 2023   Kazi ya kufanya likizo kwa mwaka wa pili. Imetolewa tarehe 26\/11\/2023Sir Godfrey Steven   1. (a) Eleza kwa kifupi maana ya kujifunza.(b) Bainisha kazi 3 anazotakiwa kuzifanya mwalimu darasani ili kumsaidiamwanafunzi aweze kujifunza.   2. Taja vitendo 5 vinavyoweza kufanywa na wanafunzi ili waweze kupimwa namwalimu wao.   3. (a) Ili msingi wa kufundishia somo la Sayansi wa “Kutenda vitendo katikaufundishaji na ujifunzaji” ufanikiwe, ni mambo gani yanatakiwa kuzingatiwa?. (b) Nini maana ya kujifunza kwa “ujenzi wa maana”?   4. (a) Eleza maana ya kufundisha.(b) Kwa kutumia mifano, bainisha mitazamo ya ujifunzaji. (Toa mfano mmoja kwa kila mtazamo).   5. (a) Tofautisha uchunguzi wa kisayansi na jaribio la kisayansi.(b) Andika ripoti ya jaribio la kisayansi lililofanywa la kuonesha mabadiliko katika hali za maada kiumbo.   6. Eleza hatua kwa hatua namna ya kufundisha kwa njia ya jarbio ili wanafunziwaweze kuelewa.   7. Kwa kutumia michoro onesha ni nini hutokea wakatia) Mwanga unaposafiri kutoka media moja hadi nyingine zenye ujazonene tofauti b) Miale ya mwanga inapopita kwenye lensi mbinuko   8. Eleza kwa ufupi maana ya istilahi zifuatazoa) Omnivorab) Hebivorac) Kanivorad) Kinga ya mwili   9. Kuungua kwa karatasi ni badiliko la kemikali. Thibitisha kauli hiyo kwa kutoa hoja nne.   10. Gurudumu na ekseli zenye ufanisi wa 95% ilitumika kuinua mzigo wenye uzito wa 1200N. Ikiwa nusu kipenyo cha gurudumu ni sm 40 na cha ekseli ni sm 5. Kokotoa a) Uwiano wa mwendo dhahiri wa gurudumu na ekselib) Manufaaa ya kikenikac) Jitihada iliyotumika kuinua mzigo   11. (a) Maabara ni nini?b) Eleza sifa 5 za maabara borac) Taja alama tano za tahadhali za kemikali zinazotumika katika chupa za kuhifadhia kemikali mbalimbali katika maabarad) Eleza tahadhari 4 za kuchukua ili kujikinga wewe mwenyewe na ajali katika maabara.   12. Kwa kutumia mifano, bainisha njia nne zinazoweza kueneza magonjwa ya kuambukiza. 13. (a) Eleza maana ya ukinzani katika umeme(b) Taja sababu tatu (03) zinazoathiri ukinzani katika umeme, Please enter your email address","img":"https://www.quiz-maker.com/3012/images/ogquiz.png"}
Powered by: Quiz Maker