MBINU ZA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZA HISABATI
{"name":"MBINU ZA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZA HISABATI", "url":"https://www.quiz-maker.com/QPREVIEW","txt":"JISOMEE MBINU ZA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZA HISABATI 1)Taja mbinu tano unazoweza kutumia kumfundishia mwanafunzi kujumlisha, kutoa, kuzidisha, kugawanya namba nzima na namba kamili. i) Majadiliano katika vikundi ii) Maswali na majibu iii) Changanya kete iv) Onesho mbinu v) Bangua bongo 2)Eleza kwa kifupi mbinu mbili (2) anazoweza kutumia mwalimu iwapo anataka kufundisha namna ya kutafuta hasara na faida katika biashara kwa kutumia jedwali. Mbinu za kufundishia faida na hasara ni: i) Onesho mbinu ii) Majadiliano katika vikundi - Kwa kutumia onesha mbinu, kuwaongoza wanafunzi namna ya kupata hasara na faida katika biashara kwa kutumia jedwali. Hapa wanafunzi wanakuwa wafuatiliaji wa kile kilichofanywa na mwalimu ubaoni. - Kwa kutumia majadiliano katika vikundi, kuwaongoza wanafunzi kwa kuwapa maswali tofauti tofauti ya faida na hasara wajadiliane kwa kufanya kama mwalimu alivyoonesha ubaoni. 3)Jibu maswali yafuatayo A)Taja sehemu mbili ambazo majira ya nukta yanaweza kutumika. B)Fafanua mbinu tano (5) zinazofaa kufundishia urefu, ujazo na wakati katika shule za msingi Majira ya nukta hutumika katika sehemu zifuatazo: i) Katika shughuli za ujenzi ii) Katika shughuli za mawasiliano Mbinu zinazofaa kufundishia urefu, ujazo na wakati. i) Onesha mbinu Mbinu hizi hutumika katika hatua za awali katika uwasilishaji wa urefu au ujazo kwa kuwaongoza wanafunzi kutambua urefu ni nini na ujazo ni nini kwa maandishi au michoro. ii) Michoro na picha Mbinu hizi hupelekea mwalimu kuandaa michoro na picha za urefu na ujazo wa maumbo tofauti tofauti ili kukazia maarifa mapya kwa wanafunzi kuhusu mada husika. iii) Majadiliano katika vikundi Katika mbinu hii mwalimu anapaswa aandae maswali ya kutosha kuhusu urefu, ujazo na wakati yatakayopelekea kuruhusu mjadala baina ya wanafunzi. Ili yaweze kuleta mjadala yanapaswa kuwa na changamoto kidogo itakayomfanya mwanafunzi afikirie kidogo. iv) Bangua bongo Mbinu hizi hutumika na mwalimu kwa kuruhusu majibu ya mdomo kutoka kwa wanafunzi. Mfano mwalimu anaweza akaandaa maswali ya wakati na kuuliza wanafunzi wabadilishe katika mtindo wa saa kumi na mbili au ishirini na nne lakini pia kutaja kanuni za kutafuta ujazo wa miche tofauti tofauti. v) Changanya kete Mbinu hii hutumika kwa kuwapa nafasi wanafunzi juu ya uundaji wa kanuni za ujazo wa miche tofauti kwa kuunganisha mawazo miongoni mwao kwa kuhama kutoka kundi moja kwenda jingine kwa ajili ya kujadili mada moja ili kufikia lengo. 4)Eleza kwa kifupi mbinu nne (4) zinazofaa kufundishia matendo katika sehemu. Zifuatazo ni mbinu zinazofaa kufundishia matendo katika sehemu. i) Onesho mbinu Ni mbinu inayompa muda mwingi mwalimu kuwasilisha maarifa mapya kwa wanafunzi. Hutumika baada ya kupata maarifa ya awali ya wanafunzi ili kuboresha zaidi maarifa yao. ii) Majadiliano katika vikundi. Mwalimu anapaswa kuandaa maswali yatakayoweza kufanywa darasani na wanafunzi kupata mwongozo juu ya maswali waliyopewa. iii) Maswali na majibu Maswali haya yanaweza kuwa miongoni mwa wanafunzi wenyewe au mwalimu na wanafunzi. iv) Changanya kete Mbinu hii hufanyika kwa kuwachanganya wanafunzi wa makundi tofauti tofauti ili kuboresha mawazo juu ya mada fulani miongoni mwa wanafunzi wenyewe wakiongozwa na mwalimu. 5)Fafanua mbinu tano (5) zinazofaa kutumika katika kufundishia majira ya nukta katika shule za msingi. Mbinu zinazofaa kufundishia majira ya nukta. i) Mifano halisi Mbinu hii hutumiwa na mwalimu baada ya kuwasilisha maarifa mapya kwa wanafunzi kwa kutumia mifano jinsi ya kuonesha nukta au kuunda maumbo kwa majira ya nukta. ii) Michoro na picha Mbinu hizi hutumika hasa katika kipengele cha kuchora michoro ya maumbo bapa kwa kuunganisha nukta za majira ya nukta. iii) Uvumbuzi Mbinu hii hutumika kwa kuwapa maswali ya nukta na kuwasilisha nukta hizo kwa kutumia majira ya nukta na kubaini aina za maumbo bapa yatakayopatikana kutokana na muunganisho wa nukta hizo. iv) Majadiliano katika vikundi Mwalimu anapaswa kuwapa maswali yatakayowapa changamoto ili kuruhusu majadiliano ili kufikia lengo la kutatua changamoto ya maswali waliyopewa. v) Kualika mgeni Mbinu hii hutumika na mwalimu ili kuwateka kimawazo wanafunzi kwa kumualika mwalimu wa somo kama unalofundisha kwa ajili ya kufundisha mada fulani. Mbinu hizi huwajengea hali ya utulivu wanafunzi na kumsikiliza kwa umakini mwalimu aliyealikwa. 6)Fafanua tofauti zilizopo kati ya dhana za numerali na tarakimu. Numerali – Ni tarakimu moja au muunganiko wa tarakimu zaidi ya moja. Mfano :- 9,99,999,9999. Tarakimu – Ni namba moja moja Mfano :- 1,2,3,4,5. 7)Onesha hatua za kugawanya desimali kwa desimali. Tumia mfano huu 0.033÷0.03 8)Mwanafunzi mmoja alijibu maswali kama ifuatavyo Onesha maeneo mawili ambayo mwanafunzi huyu anahitaji msaada. Huyu mwanafunzi anahitaji msaada katika kuzidisha namba inayozidi nafasi ya tarakimu. MFANO 46 x 2 6 x 2 = 12 12 imezidi nafasi ya mamoja hivyo namba mbili itabaki katika nafasi ya mamoja na moja itajumlishwa baada ya kuzidisha (4×2) kuwa 9. 46 x 2 92 88 x9 8 x 9 = 72 Namba mbili itabaki katika nafasi ya mamoja na saba itajumlishwa baada ya kuzidisha (8×9) kuwa 79 88 x 9 792 9)Orodhesha vipengele vinane (8) vya azimio la kazi. Vipengele vya azimio la kazi i) Ujuzi ii) Lengo iii) Vitendo vya ufundishaji iv) Vitendo vya ujifunzaji v) Zana\/vifaa vya ufundishaji vi) Rejea vii) Upimaji viii) Maoni 10)Eleza mambo mawili muhimu ya kuzingatia wakati wa kutathmini somo la Hisabati. (i) Kutambua makuu yanayopaswa kufundishwa. (ii) Kupata mrejesho wa mambo wanayopaswa kujifunza. 11)Nyota zimepangwa katika mafungu kama ifuatavyo 12) 13)Bainisha hatua utakazozifuata kuwaongoza wanafunzi kutafuta thamani ya (a)(i) Hatua ya kwanza Kuwaongoza wanafunzi kutambua mahusiano yaliyopo baina ya vizio vya km, hm, dm. Km 1= hm 10 Hm 1= m 100 (ii) Hatua ya pili Kuwaongoza wanafunzi kuzidisha na kuweka jibu lote bila kuhamisha tarakimu. km hm m 7 9 200 x 6 42 54 1200 (iii) Hatua ya tatu Kuwaongoza wanafunzi kuhamishazi kiasi kilichozidi kutokana na mahusiano ya vipimo. km hm m 7 9 200 x 6 47 5 200 (b) (i) Hatua ya kwanza Kuwaongoza wanafunzi kutambua mahusiano yaliyopo baina ya vizio vya m, dm, sm m1 = dm 10 dm 1= sm 10 (ii) Hatua ya pili Kuwaongoza wanafunzi kugawanya na kuhamisha baki inayozidi kulingana na mahusiano yaliyopo baina ya vizio. 14)Fafanua faida mbili za kutumia njia ya jozi katika kufundishia Hisabati. (i) Hukuza stadi za ubunifu na mawasiliano baina ya wahusika (ii) Husaidia kujenga kumbukumbu kwa wanafunzi","img":"https://www.quiz-maker.com/3012/images/ogquiz.png"}
More Quizzes
Simpsons Voice Actors
840
20100
GIT infection 1
1580
Arrange in sequence
100
Ace the Museum OSRS: International Museum Trivia
201023587
Linear Equations in Two Variables: Are You Ready?
201029232
Free Mako Mermaids Characters - Find Your Mermaid Match
201023587
Test Your Southern Miss Golden Eagles Football Roster IQ
201046601
Which Holiday Are You? Discover Your Festive Side
201022893
Free Management Control
201021225
Free Commercial Property Knowledge
201021648
Think You Know FTCE English 6-12? Take the Free!
201029861