JOINING INSTRUCTIONS
{"name":"JOINING INSTRUCTIONS", "url":"https://www.quiz-maker.com/QPREVIEW","txt":"MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA CHUO CHA UALIMU ILONGA 2022 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA TEL:+255-23-2623025 CHUO CHA UALIMU ILONGAFAX: +255-23-2623451 S.L.P 98RES: 2623339 KILOSAEmail:ilongatc@gmail.com 17.05.2022Phone 0755536679 1. UTANGULIZI:Ninayo furaha kukujulisha kuwa umechaguliwa kujiunga na mafunzo ya Astashahada ya Ualimu katika Chuo cha Ualimu Ilonga. HONGERA SANA. Hii ni bahati ya pekee kwako kuwa mmojawapo wa wanachuo watakaopatiwa mafunzo ya astashahada ya Ualimu katika Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA MIWILI. DIRA YA CHUO: Kuwa chuo kinachoongoza kitaifa katika kuandaa walimu bora na mahiri kwa manufaa ya Taifa. DHAMIRA YA CHUO: Kuandaa mazingira mazuri ya kujifunza na kufundishia, kuendeleza walimu kitaaluma na kitaalamu kwa kutumia sayansi na Teknolojia, pia kuhifadhi tunu za Taifa. MOTO WA CHUO: \"Elimu ni Uwezo\".(Education is Power) MAHALI CHUO KILIPO.Chuo cha Ualimu Ilonga kipo mkoani Morogoro, wilaya ya Kilosa umbali wa kilometa 9 kaskazini mwa mji wa Kilosa. Maeneo ya kupandia basi kwa wale wanaotoka Dodoma, Singida, Mwanza, Tabora, Shinyanga n.k, kituo ni Dumila . Msamvu Morogoro Kwa wale wanaotoka Dar es salaam, Tanga, Iringa, Moshi, Arusha n.k, watapanda mabasi Msamvu-Morogoro. Kituo utakachoteremkia ili kuelekea chuoni ni Ilonga Msalabani umbali wa kilometa moja toka hapo. Unaweza kutembea kwa miguu au kupanda pikipiki(Bodaboda), kwa kiasi cha Tsh 1000\/=. Endapo utatokea Kilosa mjini, utalipa kiasi kisichozidi Tsh 4000\/= kwa bodaboda, ikiwa utapanda gari nauli haitazidi Tsh 3000\/= ⦁ MAHITAJI YA USAJILI. ⦁ Vyeti Na VitambulishoIli uweze kusajiliwa Chuoni, utatakiwa uje na vyeti halisi na nakala zifuatavyo:- ⦁ Cheti halisi cha matokeo ya mtihani cha Elimu ya sekondari kilichotolewa na Baraza la mitihani la Tanzania (CSEE) ⦁ Cheti cha kumaliza Elimu ya Sekondari (Leaving certificate) ⦁ Hati ya matokeo(Result slip) kwa waliomaliza kidato cha nne katika mwaka 2021. ⦁ Cheti halisi cha kuzaliwa ⦁ Ada:Ada ya chuo ni Tsh 450,000\/= kwa mwaka. Malipo yote ya ADA wasiliana 0785786165, 0784975131 , 0769142988 Ili upatiwe CONTROL NUMBER ya kulipia fedha hizo za Ada. ⦁ Michango Kila mwanachuo, atatakiwa kuchangia michango kama ifuatavyo : MICHANGO JUMLA KWA MWAKA Usajili na kitambulisho 20,000 Mara moja tuu Ukarabati 25,000 kwa mwaka Serikali ya wanachuo 5000 kwa mwaka Usafi, mazingira na EK 20,000 kwa mwaka Kukodisha Godoro 10,000 kwa mwaka Ulinzi 30,000 kwa mwaka Michezo 30,000 kwa mwaka Huduma ya kwanza 10,000 kwa mwaka JUMLA 150,000 Fedha yote ya MICHANGO ilipwe kwenye akaunti ya NMB, namba 21803100001 Jina la akaunti ni Local Ilonga Teachers’ College. Tafadhali andika jina la mwanachuo anayelipiwa\/anayelipa. NB: -Tafadhali usichanganye fedha ya Ada na michango kwenye akaunti moja.Soma maelekezo yaliyotolewa hapo mwanzo ya namna ya kulipia ADA- Uje na nakala za malipo ya benki (pay in slips) kuthibitisha malipo. Nakala tatu za risiti ya malipo ya MICHANGO YAKO. Unaweza kulipa nusu kwa kila muhula HAKIKISHA UNAKUJA NA BIMA YA AFYA AU Tsh 50,400 SARE YA CHUO.Kila mwanachuo anatakiwa KUJA na sare kama ifuatavyo. (i ) WANAWAKE:⦁ Mashati mawili mikono mirefu-Light Blue⦁ Sketi nyeusi mbili za heshima (urefu unaopita magoti kwenda chini ) Mshono wa moja kwa moja wenye mpasuo wa kufunika nyuma (overlaping), kitambaa kiwe cha suti ya kiume kisicho na mng’ao wala mistari,⦁ Viatu vyeusi vyenye visigino vifupi,⦁ Tai nyeusi,⦁ Koti jeusi,⦁ Soksi kijivu,⦁ Kwa wanachuo Waislam watavaa suruali nyeusi, nusu kanzu (panjab) ya rangi ya bluu bahari na juba nyeusi isivuke vitanga vya mikono,⦁ T-Shirt yenye nembo ya chuo ni lazima uwe nayo inapatikana Chuoni. Uje na Tsh. 20,000\/= . ⦁ WANAUME:⦁ Mashati mawili mikono mirefu – Light Blue,⦁ Suruali mbili nyeusi zenye malinda mawili kila upande wa mbele mfuko mmoja nyuma, (Angalia mchoro ulioambatishwa)⦁ Viatu vyeusi vya kufunika miguu,⦁ Tai nyeusi pana na ndefu,⦁ Koti jeusi,⦁ Soksi kijivu ,⦁ T-Shirt yenye nembo ya chuo ni lazima uwe nayo inapatikana Chuoni. Uje na Tsh. 20,000\/= . PIA Wanachuo wa kiislamu waje na nguo maalumu kanzu kwa wavulana na baibui nyeusi kwa wasichana kwa ajili ya matumizi ya siku ya Ijumaa watokapo nje ya chuo kwenda kwenye ibada ya Ijumaa. NB : Mchoro wa sketi na suruali vimeambatanishwa na fomu hii. 3:1 Sare za MichezoNjoo na Track-suit jozi moja ya rangi ‘Dark blue’(ADIDAS) T-shirt ( jezi ya bluu isiyo na nembo\/jina la timu yeyote), (kwa wavulana na wasichana). Siku ya kuripoti vaa full track-suit na raba nyeupe za michezo. Bukta mbili rangi ya bluu (adidas), viatu vya mpira wa miguu ( njumu ikiwezekana) – wavulana, skintight 2 rangi nyeusi (ndefu), stocking za rangi ya bluu, raba nyeupe za kamba, sketi maalumu za michezo (special) kwa wasichana ni lazima uje na vifaahivyo 4.0. MAHITAJI YAKO MUHIMUUje na vitu vifuatavyo ;- shuka mbili nyeupe, foronya mbili nyeupe, shuka mbili rangi yoyote, mto mmoja, na chandarua nyeupe kwa ajili ya kuzuia mbu, Ndoo za kufulia na kutunzia maji ya kunywa. 5.0 MAHITAJI YA TAALUMAUje na vitu vifuatavyo : daftari 10 (counter book quare 2) na Msomi 10, mathematical set, penseli HB, mafaili 03 (flat files), rula ya sm 30 na kalamu za kutosha. Vifaa hivi vinapatikana kwenye maduka yaliyopo jirani na Chuo. Aje na vitabu angalau vitatu (03) vya masomo yanayofundishwa shule za msingi Tanzania. 6.0. AFYAUje na fomu iliyojazwa na daktari wa wilaya au mkoa baada ya kuthibitishwa afya yako (fomu imeambatanishwa). Endapo una ugonjwa wa kudumu njoo na vyeti pamoja na dawa ambazo huwa unazitumia. Uje na Tsh 50,400 kwa ajili ya BIMA YA AFYA KAMA HUNA. ⦁ MAHITAJI MENGINEUtatakiwa kuja na;-Vyombo vya kulia chakula kama vile sahani, kikombe, vijiko, umma n.k, galoni ya maji yenye ujazo wa lita (5) tano kwa ajili ya maji ya kunywa, ndoo ya ujazo wa lita (10) kumi au zaidi (vifaa hivi vinaweza kupatikana kwenye duka la Chuo), Uje na fedha za kutosha kwa matumizi yako binafsi. Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba 0784975131, 0754633301, 0784705316, 0652838127 8:0. Mwanachuo ambaye hatakamilisha maagizo yote HATASAJILIWA.Siku ya kuripoti vaa full track-suit na raba nyeupe za michezo ili upokelewe. NB: Utakapofika chuoni uje na fomu hii.⦁ Unatakiwa kuripoti chuoni kuanzia tarehe 13.06.2022 mwisho wa kuripoti ni tarehe 20.06.2022 baada ya hapo hutapokelewa chuoni.⦁ Usije na sanduku kubwa au zaidi ya moja. Nguo za nyumbani zinahitajika chache. Unaweza pakua form hii nzima ikiwa na viambatanisho vyake vyote kwa kubonyeza button ya download hapo chini.","img":"https://www.quiz-maker.com/3012/images/ogquiz.png"}
More Quizzes
Adventuring Occupation
5220
What current nba player r u (2021)
7440
Authors and Book Titles
15819
210
Am I Jealous: Discover Your Jealousy Triggers
201026361
Ultimate Tokio Hotel: Test Your Band Knowledge
201045747
Master French Plurals: Free to Boost Your Skills
201042433
Ace the Parts of a Book & Their Meanings
201025877
Is Your Friend a Jerk? Take the 'Jerk Friends'!
201030156
Can You Ace the Inconvenience Yourself Day?
201035590
Free Leadership & Emergency Size-Up Knowledge Test
201024757
Free EMT Final Exam Practice Test
201021265