TWAALIBAATUL ILMU
Quiz Week 74/5 - Twaalibaatul Ilmu

Asbabu nnuzul ya aya ya 33 ifuatayo, nani walokusudiwa kuwa Ahlil Bayt Rasul (SwallaAllahu alayhi wasallam)?
"Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani. Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na kukusafisheni baarabara."
Wake wa Mtume (SwallaAllahu alayhi wasallam)
Watoto wa Mtume (SwallaAllahu alayhi wasallam)
Ahlil Kisaa (Sayyidatina Fatma, Sayyidna Ali, Hassan na Hussain)
Ahlil Jaffar, Aqeel na Abbas
Kwa hadithi ilopokewa na Sayyidatina Aisha na Ummu Salama radhi za Allah ziwashukie wao, (Mtume (SwallaAllahu alayhi wasallam) aliwaingiza nani katika kishamiya chake na kuomba kutakaswa kwao kutokana na machafu?
 
Sayyidatina Fatma, Sayyidna Ali, Hassan na Hussain ( radhi za Allah ziwashukie wao)
Wake wa Mtume (SwallaAllahu alayhi wasallam)
Swahaba wote wa Mtume (SwallaAllahu alayhi wasallam)
Sayyidatina Aisha na Ummu Salama (radhi za Allah ziwashukie wao)
Allah (subhana wa taala) husamehe madhambi ya mja pindi anapo omba taubatan nnasuha, ni mtu gani asiye taqabaliwa tauba yake?
Mtu mzima mzinifu
Muuwaji
Mshirikina
Maskini mwenye kibri
Katika aya ya 35, Allah (subhanahu wataala) amewaandalia msamaha na ujira mkubwa watu gani? Taja aina ya watu TISA
Waislamu wanaume na Waislamu wanawake
Waumini wanaume na Waumini wanawake
Wat'iifu wanaume na wat'iifu wanawake
Wanao subiri wanaume na wanawake
Wanyenyekevu wanaume na wanawake
Watoao sadaka wanaume na wanawake
Wanao funga wanaume na wanawake
Wanao jihifadhi tupu zao wanaume na wanawake
Wanao mdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi wanaume na wanawake
Wanao kwenda hajj wanaume na wanawake
Wanaolisha mayatima wanawake na wanaume
Wanaume wanaopigana Jihad
Wanawake wanao kaa majumbani mwao
Wanaounga kizazi wanaume na wanawake
Maneno gani SITA swahihi yafuatayo yalijiri katika mwaka wa kumi wa hijra
Alikufa Ibrahim bin Muhammad (swallaAllahu alayhi wasalam)
Aliandaa jeshi lilokuwa chini ya Usama bin Zaid
Alimtuma Sayyidna Ali ende kwa qabila ya Yemen na akamwambia asipigane mpaka wakipigwa ndio wapigane, akafanya hilo na wakashinda vita na akawalingania watu na wakasilimu
Alimtuma Sayyidna Muadh ibn jabal Yemen ya chini
Alihiji Mtume (swallaallahu alayhi wasallam) hija yake ya mwisho
Alimtuma Sayyidna Aba Musa Al ashari Yemen ya juu
Alimtuma Sayyidna Muadh ibn jabal Yemen ya juu
Alimtuma Sayyidna Aba Musa Al ashari Yemen ya chini
Ni kipindi gani cha swala ya jamaa ya faradhi Imamu husoma Al Fatiha na sura katika rakaa mbili za kwanza kwa Jahra
Al Fajiri
Adhuhuri
Alasiri
Magharibi
Isha
Witr
Wanawake gani wawili ni haramu kuposwa
Mwenye Eda la talaka rajiiya
Mwenye Eda la kufiliwa
Mwanamke ambaye ashaposwa
Mwenye Eda la bain
Taja wasia wa nne wa Luqman Al Hakim alompa mwanawe
Kusimamisha swala
Asimshirikishe Mngu
Kutwii wazee
Kuowa mke mwenye dini
{"name":"Quiz Week 74\/5 - Twaalibaatul Ilmu", "url":"https://www.quiz-maker.com/QPREVIEW","txt":"Asbabu nnuzul ya aya ya 33 ifuatayo, nani walokusudiwa kuwa Allil Bayt Rasul (SwallaAllahu alayhi wasallam)?, Kwa hadithi ilopokewa na Sayyidatina Aisha na Ummu Salama radhi za Allah ziwashukie wao, (Mtume (SwallaAllahu alayhi wasallam) aliwaingiza nani katika kishamiya chake na kuomba kutakaswa kwao kutokana na machafu?","img":"https://www.quiz-maker.com/3012/images/ogquiz.png"}
Powered by: Quiz Maker