KAZI YA HISABATI KWA MWAKA WA I NA II WOTE

IDARA YA HISABATI
KAZI YA KUFANYA WAKATI WA LIKIZO KWA MWAKA I NA II- 2023
IMETOLEWA NA M-PAZI 28/11/2023
 
MAELEKEZO: - Katika kila swali, chagua vipengere viwili kati ya a, b au c kisha yafanye
 
1. (a) Eneo la sehemu iliyotiwa kivuli ni sm² 28. Tafuta urefu wa AB, pai = 22/7
 
(b) Mchoro ufuatao unaonesha ukuta wa jingo mojawapo la shule ya msingi
Umoja , Tafuta thamani ya w ikiwa eneo la ukuta wote ni sm² 192.
 
( c) Shule inamiliki bustani ya nyanya yenye umbo la trapeza ABCD kama
Inavyoonekana katika mchoro huu. Ikiwa eneo la sehemu iliyotiwa kivuli ni
M² 48 na urefu wa AF ni m 60, Tafuta eneo la bustani yote.
 
2. (a) Nyumba ilinunuliwa kwa gharama ya sh 150,000,000 Baada ya miaka 3 ikuazwa
kwa hasara ya 5%. Je nyumba hiyo iliuzwa kwa gharama gani?
 
(b) Katika kikapu kuna matunda 30, kati yake matunda 18 ni machungwa na
mengine ni maembe. Uwiano wa machungwa kwa maembe ni nini?
 
(c ) John ni mkubwa kuliko Mary kwa miaka 3. Na Jane ni mdogo kuliko Mary kwa miaka
2. Iwapo Jumla ya umri wao ni miaka 37, jane ana umri gani?
 
3 (a) Rebeca na Fatuma walianza kuhesabu kwa pamoja machungwa. Rebeca aliesabu kwa
Sauti kila baada ya machungwa 8 na Fatuma kila baada ya machungwa 10. Je, ni namba
Ipi moja ya kwanza wote wataitaja kwa sauti?
 
( b) Basi lina viti 23, viti viwili ni kwa ajili ya dereva na konda na 2/3
ya viti vilivyobaki
Ni kwa ajiri ya abiria. Ni viti vingapi havijakaliwa na abiria katika basi hilo?
 
(c ) Katika shamba la shule yetu, 1/3
imepandwa mahindi, 5/12 imepandwa maharage , 1/6 Imependwa mtama na sehemu iliyobaki imependwa mpunga. Onesha taarifa hizi katika
grafu kwa mduara.
 
4 (a) Katika watalii 240, 80 wanaongea kiingereza, 120 wanaongea kifaransa na 60 wanaongea
Lugha zote mbili. Je ni watalii wangapi ambao wanazungumza
(i) Kiingereza pekee (ii) kifaransa pekee
 
(b) Katika darasa , wanafunzi 15 wanapenda fizikia, 14 wanapenda kemia , 5 wanapenda
Masomo yote na 4 hawapendi masomo yote. Tumia mchoro wa venni tafuta idadi ya
Wanafunzi katika darasa hilo.
 
( c) Katika lenye wanafunzi 40, wanafunzi 20 wanapenda Hisabati na 30 wanapenda Uraia.
Tumia mchoro wa venni, tafuta idadi ya wanafunzi
(i) Wanaopenda masomo yote mawili.
(ii) Wanaopenda Hisabati pekee
(iii) Wasiopenda masomo yote mawili.


 

Tunawatakia likizo njema
{"name":"KAZI YA HISABATI KWA MWAKA WA I NA II WOTE", "url":"https://www.quiz-maker.com/QPREVIEW","txt":"IDARA YA HISABATIKAZI YA KUFANYA WAKATI WA LIKIZO KWA MWAKA I NA II- 2023 IMETOLEWA NA M-PAZI 28\/11\/2023   MAELEKEZO: - Katika kila swali, chagua vipengere viwili kati ya a, b au c kisha yafanye   1. (a) Eneo la sehemu iliyotiwa kivuli ni sm² 28. Tafuta urefu wa AB, pai = 22\/7   (b) Mchoro ufuatao unaonesha ukuta wa jingo mojawapo la shule ya msingi Umoja , Tafuta thamani ya w ikiwa eneo la ukuta wote ni sm² 192.   ( c) Shule inamiliki bustani ya nyanya yenye umbo la trapeza ABCD kama Inavyoonekana katika mchoro huu. Ikiwa eneo la sehemu iliyotiwa kivuli niM² 48 na urefu wa AF ni m 60, Tafuta eneo la bustani yote.   2. (a) Nyumba ilinunuliwa kwa gharama ya sh 150,000,000 Baada ya miaka 3 ikuazwakwa hasara ya 5%. Je nyumba hiyo iliuzwa kwa gharama gani?   (b) Katika kikapu kuna matunda 30, kati yake matunda 18 ni machungwa na mengine ni maembe. Uwiano wa machungwa kwa maembe ni nini?   (c ) John ni mkubwa kuliko Mary kwa miaka 3. Na Jane ni mdogo kuliko Mary kwa miaka 2. Iwapo Jumla ya umri wao ni miaka 37, jane ana umri gani?   3 (a) Rebeca na Fatuma walianza kuhesabu kwa pamoja machungwa. Rebeca aliesabu kwa Sauti kila baada ya machungwa 8 na Fatuma kila baada ya machungwa 10. Je, ni namba Ipi moja ya kwanza wote wataitaja kwa sauti?   ( b) Basi lina viti 23, viti viwili ni kwa ajili ya dereva na konda na 2\/3ya viti vilivyobakiNi kwa ajiri ya abiria. Ni viti vingapi havijakaliwa na abiria katika basi hilo?   (c ) Katika shamba la shule yetu, 1\/3imepandwa mahindi, 5\/12 imepandwa maharage , 1\/6 Imependwa mtama na sehemu iliyobaki imependwa mpunga. Onesha taarifa hizi katikagrafu kwa mduara.   4 (a) Katika watalii 240, 80 wanaongea kiingereza, 120 wanaongea kifaransa na 60 wanaongeaLugha zote mbili. Je ni watalii wangapi ambao wanazungumza (i) Kiingereza pekee (ii) kifaransa pekee   (b) Katika darasa , wanafunzi 15 wanapenda fizikia, 14 wanapenda kemia , 5 wanapenda Masomo yote na 4 hawapendi masomo yote. Tumia mchoro wa venni tafuta idadi ya Wanafunzi katika darasa hilo.   ( c) Katika lenye wanafunzi 40, wanafunzi 20 wanapenda Hisabati na 30 wanapenda Uraia.Tumia mchoro wa venni, tafuta idadi ya wanafunzi (i) Wanaopenda masomo yote mawili.(ii) Wanaopenda Hisabati pekee(iii) Wasiopenda masomo yote mawili.   Tunawatakia likizo njema, Please enter your email address","img":"https://www.quiz-maker.com/3012/images/ogquiz.png"}
Powered by: Quiz Maker